
Jaalia katika fikra zako kwamba: leo ni siku muruwa ya mwezi wa Septemba. Hakuna joto wala baridi, upepo mwanana unapepea na mawingu yanang’ara angani. Unachukua blanketi lako na kuelekea katika moja ya fukwe huru za jiji la Dar es salaam. Unajiandaa kwenda kujipumzisha ufukweni hapo na kufurahia machweo jua. Bali unapofika ufukweni mipango yako inatibuliwa bila ya kutegemea. Unaelezwa na afisa ulinzi kuwa serikali imeweka sheria mpya za matumizi ya fukwe. Unaambiwa kwamba huwezi kutumia ufukwe huo kwa vile wewe ni mtu mweusi. Watu wengine wowote wanaruhusiwa kutumia fukwe hizo isipokuwa watu weusi tu, na iwapo mtu mweusi yeyote angekaidi amri hiyo basi nguvu ingeweza kutumika. Continue reading “Ubaguzi mubashara: kadhia ya maadili dhidi ya uwepo wa mipaka”








