Sio Kitu: Kuanzisha mazungumzo ya falsafa ya haki za wanyama kwa Kiswahili

Namna tunavyowatendea wanyama inaonyesha kwa kiasi kikubwa utu wetu. Wanyama hawawezi kuzungumza lugha zetu, lakini wana uwezo wa kuhisi. Wanahisi maumivu, hofu, furaha na faraja—kama sisi. Wanathamini maisha yao, kama sisi tunavyothamini yetu.

Hata hivyo, kila siku wanyama wengi wanateseka. Katika mashamba, maabara, na shughuli za burudani mbalimbali, mara nyingi wanachukuliwa kama vitu tu—vitu vya kutumiwa, kudhibitiwa au kutupwa.

Ni kwa sababu hii kwamba tumeanzisha Sio Kitu.

Continue reading “Sio Kitu: Kuanzisha mazungumzo ya falsafa ya haki za wanyama kwa Kiswahili”

Mtu na Jinsia

Je, unajua tofauti kati ya utambulisho wa kijinsia, muonekano wa kijinsia, jinsia ki-anatomia, na mwelekeo wa kijinsi? Baadhi ya marafiki na mimi tumeunda kitini cha ukurasa mmoja, kulingana na Genderbread Person ya Sam Killermann, ambayo inafafanua dhana hizi kwa njia inayoweza kufikiwa na ya kuvutia. Ni zana nzuri ya kufundishia na njia nzuri ya kuanzisha mazungumzo muhimu, iwe shuleni, chuo kikuu, matukio ya kijumuiya, au warsha za utetezi. Ni bure kwa mtu yeyote kupakua na kutumia kwa madhumuni ya elimu, na kukuza uvumilivu, kuelewa, na kuthamini tofauti za binadamu.

Continue reading “Mtu na Jinsia”