
Ni janga kubwa na lisilo na kifani. Linaleta uchungu na mateso kwa wanawake na familia zao. Linaharibu jamii katika kila nchi na tamaduni. Lakini cha kushangaza, ni mara chache linazungumziwa, na kwa hakika halishughulikiwi kwa uharaka, tofauti kabisa na janga lingine lolote, ambalo limewahi kuwepo angalau kwa miaka miwili iliyopita. Tanzania ni mfano wa nchi ambayo janga hili limejikita sana lakini linafichwa. Katika nchi kama hii yenye mandhari nzuri, visiwa vya kupendeza, na wanyama wa porini wa kuvutia, kufichwa kwa janga hili kunaleta kizungumkuti.
Continue reading “Ni zaidi ya suala la familia!”